Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Yohana Sintoo amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo kuwa wabunifu na wawajibikaji katika maeneno yao ya kazi ili kuleta ufanisi katika sekta walizopo.
Ameyasema hayo kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo alipofanya kikao na watumishi wote wa halmashauri kilichokuwa na lengo la kuukaribisha mwaka mpya wa serikali.
Amesema kuwa uwajibikaji unaenda sambamba na ubunifu kwani watumishi wakiwa wabunifu wataboresha mazingira ya kazi bila kuhitaji kutumia fedha nyingi za serikali na kazi nzuri ikaonekana kwa gharama nafuu.
Katika kuzungumzia ubunifu wa kutekeleza majukumu kwa gharama nafuu, Sintoo amewapongeza watumishi wa Ustawi wa Jamii kwenye halmashauri hiyo ambao wameonesha ubunifu kwa kupendezesha mazingira yanayozunguka ofisi zao kwa michoro na ujumbe unaoendana na huduma wanazotoa.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amemwagiza Afisa Manunuzi wa halmashauri hiyo Sabiano Wambura kukamilisha kazi ya kuweka utambulisho na maelekezo ya kuonesha mahali halmashauri ilipo ili kila mtu aweze kutambua na kusisitiza kupewa utekelezaji wa kazi hiyo ndani ya siku saba.
Aidha Sintoo amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kuimarisha usimamizi wa usafi wa mazingira kwenye sehemu zao za kazi huku akiwakumbusha kuwa uchafu unapunguza ari ya kufanya kazi na mazingira masafi yanahamasisha uwajibikaji.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai