Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Elia Sintoo amewataka wafanyakazi wa Umma katika Wilaya za Hai na Siha kushirikiana kwa kutumia vyama vya ushirika kwani ndiyo suluhisho halisi la maswala ya kiuchumi.
Sintoo ameyasema hayo wakati akitoa salamu za Halmashauri yake kwenye mkutano mkuu wa 17 wa chama cha akiba na mikopo cha Hai Rural Teachers Saccoss LTD uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya chuo cha ufundi Hai.
Amewataka watumishi kutumia vizuri huduma za saccos kwani zinasaidia katika kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu na kuwataka kuacha kutumia vyama ambavyo havijasajiliwa ili kuepuka usumbufu.
Pia amebainisha wazi kuwa Halmashauri yake ipo tayari kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika na kuwataka watumishi wote wawe mabalozi wa kuwashawishi watumishi wenzao ambao bado hawajajiunga na saccoss kujiunga ili kuiongezea nguvu Hai Rural Teachers Saccoss.
Naye Meneja wa HRT Saccoss Upendo Lyatuu ameeleza kuwa chama hicho kilianza mwaka 2000 idadi ya wanachama waanzilishi wakiwa 67 kikiwa na mtaji wa Tshs. 335,000/= na hadi kufikia Septemba 2017 chama kimefikisha wanachama 2365 na mtaji wa Tshs. 6,064,652,078/= na kwamba tangu chama hadi kufikia Septemba 30, 2017 jumla ya Tshs. 24,031,015,000/= zimetolewa kama mikopo kwa wanachama
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai