Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa mchango wao kuimarisha upashanaji habari kwa kutumia redio za jamii zilizopo nchini.
Sintoo ametoa pongezi hizo kwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mkufunzi wa redio jamii Dkt. Dotto Kuhenga alipomtembelea ofisini kwake.
Sintoo amesema tangu UNESCO ianze kufanya mafunzo mbalimbali wa wanahabari wa Redio Boma Hai inayomilikiwa na halmashauri yake, yapo mabadiliko chanya yanayoonekana ikiwa ni matokeo ya mafunzo yanayotolewa.
Akizungumzia hatua walizopitiaa kuendesha masomo hayo Dkt. Kuhenga amesema kumekuwa na semina za mara kuwaongezea ujuzi waandishi wa habari na watangazaji wa Redio Boma katika masuala ya taaluma ya habari, kutafuta na kusimamia fedha pamoja na kuimarisha mifumo ya uendeshaji vituo vya redio.
Amesema wameshiriki kuwaongezea ujuzi watangazaji katika kuandaa mpango mkakati wa miaka mitano pamoja na kuainisha sera mbalimbali zinazoongoza utendaji kazi wa redio ikiwemo sera ya jinsia, sera ya fedha, sera ya jamii, sera ya kuandaa vipindi wakati wa uchaguzi na miongozo mingine inayoelekeza namna ya kutekeleza majumu kulingana na msimamo wa kituo.
Kwa upande wao watangazaji wa Redio Boma Hai wamezungumzia namna wanavyofaidika na mafunzo wanayopata kwa kuboresha utendaji kazi, kuiarisha mahusiano na ushirikiano na jamii iliyokaribu na redio pamoja na kutengeneza vipindi vinavyoendana na mahitaji ya jamii ya wasikilizaji.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai