Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amewatakia mitihani mema wananfunzi wa darasa la saba leo hii katika kipindi cha Siku Mpya Redio Boma Fm.
Ndg.Sintoo ameeleza katika wilaya ya hai kuna wanafunzi 4,382 wanoenda kuhitimu na ina jumla ya shule za msingi 126 na takribani walimu 2200 ameeleza kwa kusema ni moja ya wilaya iliyopo mbele sana kwenye swala la elimu kulinganisha na wilaya nyingine na ni kati ya Halmashauri 186 zilizopo hapa nchini Tanzania.
"Siri kubwa ya mafanikio katika swala la elimu ni pamoja usimamizi makini,ushirikiano na walimu pamoja na maafisa wa elimu katika halmashauri yetu" Sinto amesema.
Licha ya hayo bado Sintoo amebainisha kuwa kuna baadhi ya shule zisizofanya vizuri kwa kuchagua na kwamba amechagua shule tano(5) za sekondari na shule nne (4) za msingi kuzifanyia ufuatiliaji wa karibu ili kuzisaidia kuinuka kielimu.
"Sio shule za msingi tu pekee zinafanya vizuri bali hata za sekondari zinafanya vizuri mfano mzuri mwanafunzi aliyekuwa wa nne kitaifa kutoka wilaya ya hai akapewa zawadi ya pesa taslimu laki tano (500,000) kama kumuhamasisha afanye vizuri zaidi". Ameongeza Sintoo.
''Na hata kwa shule iliyokuwa haifanyi vizuri kama Longoi iliyokuwa ya mwisho kati ya shule 45 lakini kwa sasa tumeboresha miundombinu ya madarasa, nyumba za walimu na tumetoa kiasi cha shilingi milioni 64 na nina imani kabisa kwasasa itafanya vizuri''.
Aidha Sintoo ametoa rai kwa wazazi kutowaachia walimu majukumu ya kulea wanafunzi bali washiriki kuwasaidia watoto wao kulingana na changamoto zao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai