Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hai, Dionis Myinga, ameshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kazi yake ya kimapinduzi ya kuwapelekea fedha kwa ajili ya wananchi wanaotaabika kufuata umbali mrefu huduma za afya.
Amesema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Hai ndugu Said Juma Irando ,ambapo amesema ujenzi wa majengo manne na miundombinu ya majisafi na majitaka ya Kituo cha Afya Chekimaji, unaigharimu serikali Sh.milioni 340,000,000 na upanuzi wa majengo ya Kituo cha Afya Longoi, unaigharimu serikali Sh.milioni 400.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi wa Kijiji cha Chekimaji, vijiji vya jirani na Kata ya Masama Rundugai, kwamba serikali kupitia Wilaya ya Hai, imewasogezea maendeleo makubwa katika eneo hilo, ambako kuna majengo manne ya Kituo cha Afya Chekimaji yameshaanza kujengwa pamoja na miundombinu ya majisafi na maji taka.
Awali, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Nicetas Bongole, alisema wanategemea baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Chekimaji, utahudumia wananchi wa Kata ya Masama Rundugai na Kata jirani.
“Watu ambao tunawategemea watanufaika na huduma za afya katika Kata hii na Kata jirani ni watu takribani 19,000. Awali wananchi walikuwa wanazipata huduma hizi katika Hospitali ya Wilaya ya Hai iliyopo Bomang’ombe, kwa sababu ukanda wa tambarare ulikuwa hauna kituo cha afya,”alisema Bongole
Kuhusu Kituo cha Afya Longoi, ambacho kipo Kata ya Weruweru, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, alisema kituo hicho kimeshaanza kutoa huduma tangu Septemba mosi mwaka 2021, lakini kwa sasa kimepanuliwa kwa kuongezwa baadhi ya vitengo kama jengo la upasuaji, jengo la kufulia, wodi ya wazazi na nyumba ya mtumishi.
Kwa mujibu wa Bongole, Kituo cha Afya Longoi, kitahudumia watu takribani 13,000 wanaotoka Kata ya Weruweru, Mnadani na baadhi ya maeneo ya Kata ya Masama Rundugai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai