Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga amewataka wafanyabiashara kufanya usafi katika maeneo yanayo wazunguka ikiwa ni pamoja na vyoo.
Dionis ameyasema hayo katika Baraza la madiwani ambapo amesema kumekuwa na tabia ya utupaji taka ovyo na matumizi mabaya ya vyoo jambo mbalo limepelekea uchafuzi wa mazingira.
Hata hivyo ameyataja baadhi ya masoko kama soko la Bomba ng'ombe, sadala na mnadani miundombinu ya choo imetengenezwa vizuri lakini baadhi ya wafanya biashara wanashindwa kuitunza miundombinu hiyo.
Amesema serikali imejitahidi kutengeneza miundombinu ya vyoo masokoni ili kuweka mazingira katika Hali ya usafi hivyo ni jukumu la wafanyabiashara kuzingatia usafi wa mazingira.
Sambasamba na hayo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya hai mh. Edmund Rutalaka alizungumza swala Hilo la mazingira ambapo alisema jitihada zinafanyika kuhakikisha gari la taka linafikisha uchafu sehemu husika.
Baraza hilo la madiwani limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwa ni pamoja na Katibu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai