Mkurugenzi Sintoo Ahimiza Nidhamu Watumishi Wananchi Ofiisi za Umma
Imetumwa: March 1st, 2021
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kudumisha nidhamu wakati wa kuwahudumia wananchi kwani wananchi hao ndiyo waajiri wa watumishi wa Umma.
Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha watumishi wa makao makuu ya halmashauri hiyo Sintoo amesema anataka kuona nidhamu inaongoza halmashauri yake kuanzia kwa watumishi wanaotoa huduma hadi kwa wananchi wanaohudumiwa.
“Afisa Utumishi nakuagiza kuweka utaratibu unaoeleweka kwa wananchi kufahamu masuala ya kinidhamu wanapoingia kupata huduma kwenye ofisi za serikali. Hatuwezi kuwa tupo hapa tunawaelekeza watumishi aina ya mavazi ya kuvaa huku wananchi wakionesha utovu wa nidhamu kwa mavazi na vitendo”
“Kuna mtu unamkuta anaingia kwenye ofisi za serikali amevaa pedo na kandambili. Hii siyo sawa, watu wafike ofisini wakiwa wamevaa kiheshina ili nidhamu ya ofisi ionekane” Ameongeza Sintoo.
Aidha, Sintoo amewataka watumishi kutoa huduma bora kwa wananchi hasa waliovaa kiheshima na kuendelea kuwaelimisha wale watakaokuwa wamevaa vibaya bila unyanyapaa ili kuweka uelewa wa pamoja kuhusu masuala yanayohudu nidhaaaaaami