MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai amewashauri wanawake wa Wilaya ya Hai kuanza kujitokeza kuwania fursa za kiuchumi pale zinapojitokeza kwani maendeleo hayabagui jinsia ya mtu.
Kauli hii imesemwa kwenye hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri iliyowasilishwa kwa niaba yake na Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi Edward Ntakiliho kwenye tukio maalumu za uzinduzi wa Baraza la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi liliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri wilayani Hai.
Amesema, kwa muda mrefu sana wanawake wamekuwa hawapati nafasi za kutosha kwenye fursa za kiuchumi zilizopo kwenye jamii na kuwataka wanawake kuanza kujitokeza katika kuwania fursa hizo kwa manufaa ya familia zao na taifa kwa ujumla.
Baraza la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi la Wilaya ya Hai limezinduliwa leo ikiwa ni namna ya kuwapa wanawake nafasi ya kukutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu uchumi ikiwa ni pamoja na kupeana taarifa za fursa za uwekezaji na kupata mitaji pia kubadilishana uzoefu pamoja na bidhaa na kujadili namna ya kuboresha hali ya kiuchumi wa wanawake katika ngazi ya wilaya.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai