Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amewataka watumishi wa Umma kwenye halmashauri yake kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia sheria, miongozo na taratibu za kazi na zaidi kuheshimiana wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Sintoo amesema hayo mapema leo Desemba 2 kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo wakati wa kikao cha asubuhi na watumishi wa makao makuu ya halmashauri hiyo.
Amewataka watumishi kuweka mbele heshima kwa wananchi wanaowahudumia ili kuonesha thamani ya kazi wanazofanya lakini pia kuheshimiana wao kwa wao ili kuongeza ufanisi wa kazi.
“Niwaambie ndugu zangu, hizi kazi tunatakiwa kuzifanya kwa kuheshimiana wakati wa kutekeleza majukumu yetu; ni jambo la msingi sana”.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Idara ya Ardhi Jacob Muhumba amewakumbusha wakuu wa idara kushiriki kwenye ziara za viongozi mbalimbali wanaotembelea halmashauri yao ili kuweza kupokea maelekezo lakini pia kutoa ufafanuzi sahihi wa masuala yatakayojitokeza.
Naye Afisa Utumishi wa wilaya ya Hai Sallema Kentigern amewakumbusha watumishi kuzingatia sheria na taratibu za utumishi wa Umma ikiwemo sheria ya mavazi ili kuwa nadhifu wakati wa kuwahudumia wananchi.
Aidha amewataka wakuu wote wa idara na vitengo kuwa na nakala ya waraka wa mavazi watakaoutumia kuwaelimisha watendaji walio kwenye mamlaka zao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai ameweka utaratibu wa kukutana na watumishi wote wa makao makuu ya halmashaur kila siku ya Jumatatu kuanzia saa moja nanusu hadi saa mbili kamili ambapo idara na vitengo huwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi kwa wiki iliyokwisha na mipango ya kazi kwa wiki inayoanza utaratibu ambao umesaidia watumishi wote kufahamu mambo yanayotekelezwa na idara na vitengo mbalimbali.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai