Mkuu wa shule ya sekondari Wasichana ya Machame ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka kipaumbele katika swala zima la kuongeza na kuimarisha miundombinu ya shule.
Amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa ujenzi wa mabweni 2 na madarasa katika shule hiyo inayogharimu kiasi cha shilingi 372,600,000/.
Pamoja na shukani zako mkuu huyo wa shule ameelezea changamoto ya eneo hiyo ambalo limetumia gharama kubwa kwenye ujenzi wa msingi.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ameelezea kuridhishwa na ujenzi unaoendelea katika miradi hiyo na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuandika barua ili kuelezea changamoto hiyo ya inayotokana na jeografia ya eneo hilo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai