Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu ameelezea kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa madarasa 10 unaotekelezwa na fedha kutoka serekali kuu wilayani Hai mkoani humo utakaogharimu ya shilingi 200.
Babu ameyasema hayo katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba hivyo iliofanyika katika shule za sekondari Longoi, Hai na Mukwasa ziliyo Hai mkoani Kilimanjaro.
‘’Yaani sitaki niseme uongo nimetembelea madarasa 6 kati ya 10 yanayojengwa Hai nimefurahishwa na kuridhiswa na kasi ya ujenzi kwenye mkoa wangu kwasababu nimeanzia wilaya ya Hai na wamefanya vizuri na mwanzo ndio unaokupa picha kamili ya hali ilivyo nimatumaini yangu kuwa na huko ninakokwenda Siha, Rombo, Mwanga, Same Moshi mjini na vijijini nao watakuwa wamefanya vizuri kama wenzao wa Hai’’.amesisitiza Babu
Babu pia amewataka wakurugenzi wote kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kama ilivyo kusudiwa na kuzuia mianya yote ya matumizi yasiyofuta taratibu na sheria ya matumizi ya fedha za Umma.
‘’Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatafuta fedha hizi kwa tabu sana kwa kuhakikisha watanzania wanapata elimu bora, hizi sio fedha za kufanyia mchezo na sio fedha za kupanga matumizi mengine zijenge madarasa na kuhakikisha yanakamilika kwa muda ulioelekezwa” amesisitiza Babu.
Mkuu huyo wa Mkoa pia amewataka wazazi kushikiana na serikali kwa kumuunga mkono Rais wa Jamuuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kwa kuchangia katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kusimamia vema utekelezaji wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hai Dionis Myinga amemshukuru Rais kwa fedha hizo huku akiongeza kuwa madarasa hayo yatakamilika katika muda uliopangwa.
Amesema pamoja na miradi hiyo kuna miradi mingine mingi inayotekelezwa na fedha za mapato ya ndani na kuongeza kuwa kwa mwaka huu pekee wilaya ya Hai imetenga zaidi ya milioni 825 ya mapato ya ndani kwa shuguli za kimaendeleo.
‘’Ukienda shule ya sekondari Mnadani kuna madarasa mawili, vyoo kwenye soko la maiputa, tumekarabati choo kwa sadala sokoni, shule ya msingi Nsongoro tumejenga madarasa manne kwa zaidi ya milioni 80, ukamilishaji wa sekondari ya Shirimatunda lakini pia shule ya msingi Lambo tunamalizia ujenzi wa matundu 24 ya choo pamoja na miradi mingine mingi vyote hivyo vinafanyika kwa kutumia mapato ya ndani wilaya ya Hai hivi sasa kazi kubwa inafanyika kwa kutumia fedha kutoka serekali kuu na mapato ya ndani ya Halmashauri” ameongeza Myinga.
Mkoa wa Kilimanjaro umepokea zaidi ya bilioni 2 za ujenzi wa madarasa 125 kutoka serekali kuu huku wilaya ya Hai ikiwa imepokea kiasi cha shilingi 200 kati ya hizo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 10.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai