Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu ameipongeza wilaya ya Hai kwa kukamilsha ujenzi wa madarasa 10 ya sekondari ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora huku akizitaka halmashauri zingine kujifunza Hai.
Akizungumza katika makabidhiano ya madarasa hayo yaliyofanyika leo Disemba 13, 2022 katika Shule ya Sekondari Hai, Babu ameipongeza halmashauri hiyo kwakutumia kiasi cha fedha kilichotolewa na serikali kwa kujenga madarasa yenye viwango sahihi yapatayo 10 na ofisi za waalimu katikati.
Pia Mkuu huyo wa Mkoa ametoa maagizo kwa halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa mwezi januari wanafunzi wote wanaotakiwa kuendelea na masomo wanafanya hivyo mara moja kwani serikali imejenga madarasa hayo kwaajili ya wanafunzi hao na kinyume na hapo serikali itachukua hatua kali kwa wale wote watakao kwamisha wanafunzi kujiunga na masomo mwakani.
Aidha ameagiza Halmashauri hiyo ya Hai na halmashauri zingine katika mkoa wa Kilimanjaro kutumia fedha za ndani za Halmashauri kukarabati madarasa chakavu huku akiwapongeza wananchi waliojitolea michangango yao mbalimbali ili kununua marumaru kwa ajilia kuongeza ubora wa majengo hayo.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa wilaya ya Hai Juma Irando amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za ujenzi wa madarasa katika wilaya ya Hai jambo ambalo limetatua tatizo la pungufu wa madarasa na kwamba wanafunzi wote watakaochagulia kujiunga na elimu ya sekondari katika wilaya ya Hai hawatakosa nafasi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, Edmund Rutaraka amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha nyingi za mradi katika wilaya ya Hai, hasa katika sekta ya Afya, barabara, Maji na elimu.
“Hii shule ina bahati kuanzia mwaka 2020 hadi sasa tumejenga madarasa 11, tulianza na madarasa mawili, tukajenga madarasa sita na sasa tumejenga madarasa matatu kwa hiyo tunaweza kusema tuna shule ndani ya shule”amesisitiza Rutaraka
Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai Wang’uba Maganda amesema serikali imeamua kuwekeza kwenye mambo ya maendeleo hasa huduma muhimu za kijamii na muda si mrefu changamoto nyingi za kijamii zitakuwa zimetatuliwa.
“Tunamshukuru sana mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kwa kujali sana suala la kijamii hasa elimu, maji na barabara, watu wa Hai tunashukuru sana na tunazidi kumuombea kwa Mungu”amesema Maganda
Awali akisoma taarifa ya ujenzi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Juma Irando, Mkuu wa divisheni ya Elimu Sekondari Julius Mduma amesema wilaya ya Hai ilipokea milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 10 katika shule za Rundugai darasa moja, Hai madarasa matatu, Mukwasa darasa Moja, Neema darasa moja, Tumo darasa moja, Longoi madarasa mawili, na Roo darasa moja.Ujenzi wa madarasa yote umekamilka tayari kwa kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Januri 2023.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai