Halmashauri ya wilaya ya Hai imepongezwa kwa kuwa miongoni mwa halmashauri zinazofanya vizuri katika mkoa wa Kilimanjaro kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo usimamizi wa miradi.
Pongezi hizo zimetolewa leo na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kagaigai alipohudhuria kikao cha baraza maalum la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Hai kilichoketi kwa lengo la kupitia na kujadili hoja zilizoibuliwa na mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG).
Kagaigai amesema kuwa miongoni mwa Halmashauri zinazofanya vizuri katika mkoa wa Kilimanjaro ni pamoja na halmashauri ya wilaya ya Hai ikiwa ni pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo unaoendana na maelekezo ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.
Pamoja na pongezi hizo mkuu wa mkoa amewataka watendaji wa Serikali pamoja na madiwani wa Halmashauri hiyo kujikita katika kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato ikiwemo kuitumia Redio Boma Hai fm kama njia nzuri ya kuhamasisha ukusanyaji wa mapato hayo.
Naye mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga ameahidi kuendelea kushirikiana na watumishi pamoja na madiwani katika kusaidia shughuli za maendeleo ndani ya wilaya hiyo ili kufikia malengo ya serikali.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Hai Juma Irando ametumia kikao hicho kuwahamasisha viongozi pamoja na wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na makazi linayotarajiwa kufanyika Agost 23 mwaka huu lengo likiwa ni kuisaidia serikali kupanga mipango yake kulingana na takwimu sahihi za watu.
Halmashauri ya wilaya ya Hai ni miongoni mwa Halmashauri zenye hoja chache katika ripoti ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai