Wito umetolewa kwa makarani wa sensa kutotembea na vishikwambi sehemu za starehe ili kuzuia upotevu wa vifaa hivyo muhumu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu wakati kamati ya sensa ya mkoa ilipofika nyumbani kwa shekh wa mkoa huo shekh Mlewa Shaabani.
“Kw makarani kwanza muwe makini kwa sababu vile vishikwambi serekali imeingia gharama kubwa waache kwenda navyo maeneo ya starehe wakishamaliza kazi ni vizuri wakirudi nyumbani wakaifadhi vishkwambi na vitu vingine ndipo waendelee na mambo yao mengine”
Awali akizingumzia mwenendo wa zoezi la sensa katika mkoa na wilaya Hai Babu amesema zoezi linaenda vizuri huku akitoa wito kwa makarani kuakikisha walemavu wanasaidiwa ipaswavyo na kupewa kipa umbele ikiwa ni pamoja na kutumia wataalamu wa lugha za alama ili kuakikisha walemavu wanatoa taarifa zao vizuri.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai