Jeshi la Polisi wilayani Hai limepiga marufuku uchomaji wa matairi kwa kisingizio cha kusherehekea sikukuu za Krismas na Mwaka mpya kwani vitendo hivyo vinachochea uharibifu wa mazingira pamoja na kuharibu miundombinu ya barabara ambayo imejengwa na Serikali kwa kutumia fedha nyingi.
Akizungumza leo Disemba 22, 2022 kwenye kipindi cha Siku Mpya kinachorushwa na Redio Boma Hai fm, mkuu wa Polisi wilaya ya Hai SSP Juma Majatta amepiga marufuku hiyo na kueleza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuchoma matairi.
"Kuna baadhi ya watu wakati wa sikukuu hizi za mwisho wa mwaka husherehekea kwa kufanya uharibifu ikiwa ni pamoja na kuchoma matairi kwa kisingizio kwamba anasherehekea, jeshi la Polisi tunapiga marufuku, tunaona ni vyema tukawaelimisha mapema sana kwani yeyote atakayejaribu kufanya hivyo tutamchukulia hatua kali kabisa za kisheria na tutakuwa wakali kweli"
Akizungumzia upigaji wa fataki, mkuu huyo wa Polisi amewataka wale wenye mpango wa kupiga fataki hizo kufika kituo cha Polisi ili wapate kibali endapo jeshi hilo litajiridhisha kuwa mhusika anakidhi vigezo vya kupatiwa kibali hicho huku akitoa onyo kali kwa wanaomiliki silaha za moto kutojaribu kupiga risasi hewani wakati wa mikesha ya sherehe hizo ili kuepusha bugudha na taharuki kwa wananchi.
"Tunapaswa tujiridhishe ili tuweze kutoa hicho kibali cha kupiga fataki kwa zingatia pia mazingira ambayo mhusika atapigia fataki hiyo, tutakapojiridhisha na hayo pamoja na mambo mengine tuttatoa kibali, lakini vilevile tukikunyima kibali tutakueleza ni kwa nini tumekukataza kupiga hizo fataki kutokana na yale ambayo tutayabaini"
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai