Mkuu wa Wilaya ya Hai Mh Lengai Ole Sabaya amesitisha matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo zilizotolewa na Mbunge kwa kukihuka taratibu za kisheria ambayo inahitaji miradi yote inayo tekelzwa na fedha hizo kuidhinishwa kabla ya mwezi desemba kila mwaka na ameagiza zipelekwe kwenye mradi utakao saidia wananchi wengi na kuleta tija.
Sabaya ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa wa kijij cha Roo-Sinde kata ya Romu alipowatembelea kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Hivi karibuni Mbunge kupitia kamati ya mfuko wa jimbo aligawa fedha kiasi cha silingi 531,230.54 kwa kila kijiji bila kuwa na miradi halisi itakayo tekelezwa na fedha hizo jambo ambalo Mkuu wa Wilaya amesema halina tija kwani hakuna mradi wa maendeleo unao weza kutekelezwa kwa kila kijiji kwa kiasi hicho
“Kwa mujibu wa sheria ya mfuko wa jimbo kipengele namba 15 kipengele kidogo cha kwanza, inaelekeza miradi yote iidhinishwe kabla ya mwezi desemba na kwamba ikipia Desemba zitolewe kwa idhini ya Waziri wmenye dhamana ,lakini hadi kipindi hicho kinapita mbunge wenu hakujitokeza kugawa fedha hizo, badala yake anakuja kugawa fedha bila ya kuangalia mahitaji halisi ya wanachi”amesema Sabaya.
“Nimetoa maelekezo kwamba fedha hizo hazitakwenda popote , tutatafuta mradi mkubwa ambao utanufaisha wananchi wengi, hakuna kugawanya fedha za serikali kama sandakarawe,hakuna kutoa fedha za umma ambazo zinatokana na jasho lenu kisiasa kama nilivyoagiza fedha hizo zitaenda kutekeleza miradi itakayo wasaidia wananchi wengi “
Sabaya amesema fedha hizo sio za mtu binafsi kama ambavyo katibu wake ametoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii na kwamba zinatotolewa na serikali kuasidia kukamilisha au kuanzisha miradi mbali mbali kwenye jimbo na sio kugawa bila ya kujua mahitaji halisi wala miradi inayoenda kutekelezwa.
“mwaka jana umepita mziam hajaja mbunge wenu kuidhinisha ,hizi kero mnazo kutana nazo kila siku zingetatuliwa na fedha hizi, nina matatizo na namna ambavyo mmbunge anataka kuendesha mfuko wa fedha zinazotolewa na serikali kwa njia ya rimoti”
Akizungumza kwa niaba ya wanachi Mwenyekiti wa kijiji hicho Khalfan Swai ,amemshukuru mkuu wa Wilaya ya Hai kuingilia kati suala hilo na kuunga suala la fedha hizo kutekeleza mradi utakao onyesha mafanikio kwa Wilaya .
Hata hivyo mkutano wa kijij cha roo-sinde kata ya romu na mkuu wa wilaya ya hai Lemgai Ole sabaya akisikiliza na kutatua kero za wananchi papo hapo.
Lengai ole sabaya amesema hakuna kupeleka pesa za mfuko wa jimbo kijijini na badala yake pesa hizo zitapelkwa kwenye mradi mkubwa utakaowasaidia
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai