Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameahidi kufanya utafiti ndani ya siku saba ili kubaini ukweli kuhusu umiliki wa shamba la Kikuletwa Farm lililopo kata ya Masama Rundugai baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya mwekezaji wa shamba hilo.
Sabaya ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mkalama alipozungumza na wananchi hao huku akisisitiza kuwa haki itatendeka kwa pande zote mbili ili kuleta usawa katika jamii.
Aidha Mkuu wa Wilaya amemwagiza Kamanda wa Polisi wa wilaya kuhakikisha kuwa wananchi hao wanakuwa salama na kumtaka mwananchi yeyote atakayetishwa afikishe taarifa ofisini kwake na kuwataka wasiogope chochote pale wanapopigania haki .
“Kwanza OCD, watu wangu wawe salama na atakayetishwa alete taarifa ofisini kwangu; nyie mnaopigania haki yenu msiogope chochote” alisema mkuu wa wilaya.
Katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya ametoa onyo juu ya yeyote atakaye watishia wananchi na silaha yeyote na kusema kuwa atakaye fanya hivyo atashughulikiwa.
“Yeyote atakaye Tisha mtu na bastola nitamshughulikia wananchi nyie ndio mliotupa dhamana sisi ya kuongoza msitishiwe na chochote”alisisitiza mkuu wa wilaya.
Kwa upande wake mwekezaji wa shamba hilo Herman amesema kuwa yuko tayari kupitia upya mikataba hiyo ili kubaini kama kuna ubadhirifu uliofanyika ili haki itendeke kwa kila mmoja.
Hivi karibuni Wakazi wa Kijiji cha Mkalama walipeleka malalamiko katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya wakidai mwekezaji huyo kuwakodishia mashamba hayo kwa kiasi kikubwa cha fedha hali inayowapelekea kushindwa kuendeleza shughuli za kilimo ambacho ni tegemeo kwa maisha yao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai