Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amekabidhi Mifuko ya Saruji 200 na nondo Tani moja pamoja na kokoto lori moja kwa kituo cha polisi cha Boma Ng'ombe wilayani Hai kwaajili ya upanuzi wa kituo hicho.
Akikabidhi vifaa hivyo vya ujenzi hii leo may 23 2019, Lengai Ole Sabaya amemtaka mkuu wa kito cha polisi Lwelwe Mpina kusimamia vizuri matumizi ya vifaa hivyo vya ujenzi hivyo alivyo vitoa kwa jeshi hilo.
Sabaya amesema kuwa upanuzi wa kituo hicho utawarahisishia wananchi kufika na kupata huduma kwa haraka na kwa urahisi, na kuwa saidia polisi hao kufanya kazi katika mazingira rafiki na yakueleweka.
Amesema “Katika kutekeleza maelekezo ya Mh. Rais kuwasogezea huduma karibu wananchi, Kamatai ya Ulinzi na usalama na wadau wetu tumefanikiwa kupata mifuko hiyo 200,tunaenda kuchimba msingi hapa kwaajili yakujenga jengo jipyaa,sitegemei kabisa mje mniambie hata mfuko mmoja umepotea, mfuko mmoja ukipotea nitawashughulikia,nione kila kitu kwasababu mategemeo yetu hii ndio sehemu yenye nidhamu”.
Amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo unategemewa kukamilika ndani ya miezi mitatu huku yeye mwenyewe akiwa mwenyekiti wa kamati inayosimamia ujenzi huo.
“Nanimejipa kazi mimi mwenyewe kwamba mimi mwenyewe ndo mwenyekiti wa kamati hiyo ya ujenzi nimeshajiteua,kwahiyo na ndani ya miezi mitatu ujenzi uwe tayari umeshakamilika” amesema sabaya.
Aidha amewataka askari polisi wakituo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na kwakuzingatia sheria pasipo kumuonea mwananchi huku wakiendelea kuchukua hatua kali kwa mualifu kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo hicho (OCD) Lwelwe Mpina amemshukuru mkuu huyo wawila kwa mchango huo na kusema kuwa kwa sasa amekuwa mfano bora wakuigwa, huku akiahidi kuyatekeleza yale aliyoyasema na kwamujibu washeria.
Amesema “Nasisi tunakuahidi yote unayotupa tunayatekeleza, tutafata sheria kwa hivyo hatutaenda nje ya sheria tutafanya kazi sheria inavyotaka, katika wilaya yetu ya Hai naona ni kiongozi unaesimamia sheria vizuri na sisi tuko nyuma yako hatutaonea wananchi , kila mmoja afanye kazi kama kauli mbiu inavyosema hapa kazi tu”.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai