Mkuu wa wilaya ya Hai Juma Irando ameliagiza jeshi la Polisi wilayani humo kufanya oparesheni kubaini mabanda ya video almaarufu vibanda umiza ambavyo vinatumika kuonesha picha zinazokwenda kinyume na maadili ili viweze kufungiwa lengo likiwa ni kunusuru kizazi cha sasa na baadaye.
DC Irando ametoa agizo hilo jana alipozungumza na wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi wilayani humo na kutaka uchunguzi ufanyike ili kubaini vibanda hivyo na kuvifungia kwa lengo la kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto unakuwepo.
"Hivi vibanda vya video (vibanda umiza) OCD upo hapa, piteni chunguzeni na kufuatilia na kuona nini hasa kinafanyika huko, na vile ambavyo tunaona vinakwenda kinyume na maadili yetu tuvifungie "
"Kwanza sikuhizi si kila mtu ana TV yake nyumbani? Teknolojia imebadilika sikuhizi, ebu tuone kama vinatusaidia, kama havitusaidii tuvifungie, ebu fatilieni hili suala tuone ni namna gani tunaweza kubadilika kutoka kwenye mambo ya vibanda umiza na watu wawe na TV zao nyumbani ili ulinzi wa watoto uwepo"
Katika hatua nyingine amewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwa wakarimu kwa kupokea wageni na kuwalaza chumba kimoja na watoto kwani baadhi ya wageni hao huwageuka watoto na kuwafanyia ukatili wa kingono pamoja na kuwatishia wasitoe taarifa kwa mtu yoyote.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai