Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ,Juma Irando amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya Helpdesk Engineering Tanzania Limited,Iliyopewa zabuni ya ujnezi wa mradi wa uongezaji maji katika viunga vya mji wa Bomang’ombe kuhakikisha mardi huo unahaujengwi chini ya kiwango na kusisitiza kuwa lazima uendane thamani halisi ya fedha itakayotumika.
Irando ametoa agizo hilo wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao unajengwa katika kata ya Mnadani wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema nia ya serikali ni kuhakikisha inaondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo changamoto ya maji na hivyo kumtaka mkandarasi huyo kutekeleza mradi huo kwa wakati kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali.
Katika hatua nyingine Irando amemtaka mwenyekiti wa bodi ya maji ya Uroki Bomang`ombe ambao ndio wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanawapa wananchi bili za maji kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuzingatia uhalisia wakati wa utoaji wa bili hizo.
Kwa upande wake meneja wa RUWSA Wilaya ya Hai mhandisi Emanuel Mwampashi amesema awali asilimia kubwa ya wananchi wa mji wa Bomang`ombe walikuwa wakipata huduma ya maji kwa mgao lakini kukamilika kwa mradi huo kutarahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa sililimia 44.
Mwenyekiti wa bodi ya maji Uroki Bomang`ombe Elisante Kimaro amesema wao kama wasimamizi wa mradi huo watahakikisha kuwa wanasimamia mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati kulingana na muda uliopangwa.
Mradi huo wa maji ambao umegharimu Zaidi ya shilingi bilioni 3 unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 6 ambapo kukamilika kwake kutasaidia upatikanaji wa maji kwa azaidi ya asilimia 96.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai