Mkuu wa wilaya ya Hai Amiri Mkalipa amempongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa wodi daraja la kwanza unaoendelea katika hosptali ya wilaya ya Hai.
Mkalipa ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo aliofanya Februari 15,2023.
Akisoma taarifa ya mradi Mganga mkuu wa hospitali Dkt Itikija Msuya amesema ujenzi wa wodi daraja la kwanza (Private Ward) umegharimu kiasi cha milioni 210,141,322 ambapo fedha hizo zitakamilisha ujenzi wa jengo hilo.
Msuya amesema pindi jengo hilo litakapo kamilika itamaliza adha ya uhaba wa majengo kwani kumekuwa na uchache wa majengo kama vile famasi pamoja na maabara lakini pia hospitali itakuwa na hadhi ya wilaya.
Kwa upande wake diwani wa kata ya bomang’ombe Evod Njau ameishukuru serikali kwa kuendelea kuleta miradi mbalimbali na kujali afya za wananchi kwa kuwajengea majengo na kuboresha vituo vya afya.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai