Mkuu wa wilaya Hai Amir Mkalipa akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya pamoja na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri wameanza ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utaratibu wa serikali kila ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha.
Mkalipa amesema kuwa wamekagua jumla ya miradi minne ya maendeleo ukiwemo mradi wa shule ya msingi Nkwarungo,shule ya sekondari Harambee,shule ya wasichana Machame na kituo cha afya Kisiki na kwamba miradi hiyo imekamilika kwa ubora uliotakiwa.
“Leo tumetembelea miradi ya maendeleo minne katika wilaya yetu ya Hai,na huu ni utaratibu wa kawaida wakiserikali wa ukaguzi wa miradi kwa sababu ni mwisho wa mwaka wa fedha ni lazima tuhakikishe fedha zilizokuja zinatumika vizuri na kwa usahihi,lakini pia miradi hiyo inakamilika kwa ubora unaotakiwa”Mkalipa
Kwa upande wake mkuu wa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa Josia Gunda amewapongeza wasimamizi wa miradi hiyo ya maendeleo kwa kufuata ushauri wa TAKUKURU kwa kutumia mafundi wanaowafahamu kwani kwa kufanya hivyo kazi zimeenda kwa kiwango kinachotakiwa.
“lakini pia niwapongeze kwa sababu mmeweza kuzingatia ushauri tuliotoa TAKUKURU kwa kuweza kutumia mafundi mnaowafahamu na hapa tunaona matokeo ya kutumia fundi mnayemfahamu na kummudu kazi imeenda vizuri na hatudaiani”Gunda
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai