Mkuu wa Wilaya ya Hai lengai Ole Sabaya ameutangaza mwezi Novemba ya mwaka 2018 kuwa mwezi wa oparesheni maalumu ya kurudisha kodi na stahiki za serikali zinazohujumiwa na wananchi wasioutakia mema uchumi wa Nchi.
Sabaya ameyasema hayo leo kwenye kikao cha kupokea ripoti ya ukusanyaji wa mapato ambapo TRA imefanikiwa kuvuka lengo ililojiwekea la shilingi milioni 289 na kulivuka lengo kwa kufanikiwa kukusanya shilingi milioni 592 ikiwa ni sawa na asilimia 205 kwa kipindi cha mwezi Oktoba.
“Nawapongeza wananchi wote waliojitokeza na kuitikia wito wa kulipa kodi stahiki ya serikali lakini pia niwashukuru na kuwapongeza TRA, wametekeleza wajibu wao kwa uadilifu na niwapongeze kamati ya ulinzi na usalama kwa kushiriki wao kuhakikisha kodi ya serikali inakusanywa” Amesema Sabaya.
Kwa upande wake meneja wa TRA wilaya ya Hai na Siha Speciouza Oure amemshukuru Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuongoza uhamasishaji wa ulipaji kodi pamoja na kufuatilia wawekezaji waliokwepa kulipa kodi hali iliyosababisha makusanyo kupanda.
Aidha amewakumbusha wananchi kuendelea kulipa kodi kwa wakati ili kuepeuka usumbufu wa kufungiwa biashara zao pasipo sababu za lazima ikiwa ni pamoja kuendelea kutoa na kudai risiti kila wanapofanya manunuzi.
Mwezi Novemba mamlaka ya mapato TRA Wilaya ya Hai imejiwekea lengo la kukusanya mapato ya shilingi milioni 252 ambapo tayari imekusanya shilingi milioni 19 ndani ya siku mbili.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai