SERIKALI Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro imewataka wakandarasi wa barabara kufanya kazi kwa weledi na kukamilisha ujenzi kwa wakati kwa mujibu wa mkataba baina yao na Serikali ili thamani ya fedha iweze kuonekana
Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Juma Irando alitoa Agizo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya matengenezo ya barabara kwa mwaka fedha 2022/2023 inayosimamiwa na wakala wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA)ngazi ya wilaya hiyo.
Alisema wakandarasi wanawajibu mkubwa wa kutekeleza miradi kwa kiwango kinachostahili na kukamilisha kwa wakati ili jamii iweze kupata huduma stahiki na kuondokana na adha za miundo mbinu mibovu ya barabara .
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa TARURA wilayani Hai,Kaimu Meneja Mhandisi Musa Sumbwe alisema kwa mwaka wa 2022/2023 wanatekeleza mikataba sita ya matengenezo ya barabara yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 4.8.
Sumbwe alisema kati ya miradi hiyo upo mradi wa matengenezo wa barabara kwa kiwango cha lami ya Makoa Darajani- TaCRI-Mferejini unaotarajiwa kutumia zaidi ya bil 2.9 ambao unatekelezwa na Serikali kupitia fedha za maendeleo za tozo ya mafuta
Alifafanua kuwa kwa sasa kazi inayoendelea ni kupasua miamba ambapo ujenzi wa barabara hiyo unatekelezwa na mkandarasi Builders and Limeworks Ltd unaotarajiwa kukamilika April 25 mwaka 2024.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai