Mkuu wa wilaya ya Hai mheshimiwa Hassan Bomboko amewataka watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Hai kusimamia vyanzo vya mapato vilivyopo kwa weledi pamoja na kubunii vyanzo vipya vya mapato ili kukuza na kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri.
Amebainisha hayo alipokuwa akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri cha halmashauri ya wilaya ya
Hai (DCC) .
‘’ni wajibu wetu sasa kuangalia namna bora ya kuendelea kukusanya mapato ,na ili tukusanye mapato lazima tuwe na vyanzo vizuri vya mapato pamoja na kuongeza ufanisi ,weledi ,uaminifu katika ukusanyaji wa mapato ’’
Ameongeza kwa kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan ambapo amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2024\2025 zaidi ya bilioni 50 zimetumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya wilaya ya Hai na kuwataka watumishi wa kusimamia miradi ya maendeleo ili ikimalike kwa wakati na kwa ubora.
“ miradi tuliyoipata mipya ,lazima tuhakikishe miradi hii inakamilika kwa wakati lakin inakamilika kwa ubora,na ile thamani ya pesa lazima ionekane”
Naye Mkurugenzi wa wilaya ya Hai ndugu Dionis Myinga amesema kuwa vipaumbele vya bajeti ya halmashauri kwa mwaka 2025/2026 ni kuboresha mazingira bora ya kujifunzia na ujifunzaj,ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu,kuboresha huduma za afya na kinga tiba,kuin=marisha utawala bora na kubuni vyanzo vipya vya mapa
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai