Mkuu wa wilaya ya Hai Lazaro Twange ameomba ushirikiano kutoka wa wadau na wataalamu wa wilaya ya Hai ili aweze kutekeleza majukumu yake na kuwezesha wananchi kupata huduma inayostahili kwa wakati.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Ofisi kati yake na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa,Twange amesema yupo tayari kutumika kwa ajili ya wananchi muda wowote na siku yoyote hivyo kuwataka wakuu wa Taasisi Pamoja na Divisheni kutosita kuwasiliana naye.
naamini kuanzia leo, tutaanza kufanya kazi pale alipoa achia Mkalipa, naomba niwapongeze sana kwa kufanya kazi vizuri taarifa za Hai nyingi tunazijua na niombe kwa namna mlivyofanya kazi na Mkalipa naomba mfanye na hivyo hivyo na mimi”
“tufanye yale ambayo mamlaka imetarajia tuyafanye lakini kubwa wananchi waridhike na tunachokifanya, tutatembea sana kuhakikisha tunasikiliza wananchi kama ambavyo maelekezo ya Mamlka inatutaka tufanye” amesema Twange.
Akizungumza kabla ya kukabidhi Ofisi kwa Twange ,Mkalipa amewashukuru wakuu wa Taasisi,Viongozi wa dini,Madiwani,kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Timu yake kwa ushirikiano na kumsaidia kutekeleza majukumu yake.
nimejifunza mengi sana Hai ,nitaenda kufanyia kazi Arumeru.Nimejifunza namna ya kukusanya mapato na kuvuka lengo, namna ya kuwa wa kwanza kwenye lishe,namna ya kuwa na miradi bora ya miradi na mambo mengine mengi kwa kuwa Hai imekuwa ikifanya vizuri kwa kila Sekta”
Amir Mkalipa amehamishiwa wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha akitokea Hai huku Lazaro Twange akiwa amihamia wilaya ya Hai aiktokea wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai