Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Juma Irando ameishukuru taasisi ya misaada ya Al Ata'a kwa kushirikiana na Qatar Charity kwa kuweka kambi ya matibabu katika hospitali ya wilaya ya Hai kwa lengo la kutoa huduma za matibabu kwa wananchi.
DC Irando ameyasema hayo Julai 15 2022 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji msaada wa matibabu kwa wananchi na kuwezeshwa na taasisi hiyo ambayo imeweka kambi ya matibabu siku 3 bila malipo katika hospitali ya wilaya hiyo.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa rai kwa wadau wengine wa Afya walioko ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro kuona umuhimu wa kutoa huduma za Afya kwa wananchi kwani maendeleo ya taifa huletwa na jamii yenye Afya njema huku akiwataka wananchi kujitokeza kupatiwa huduma hizo.
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya misaada ya Al Ata'a Ahmed El hamrawi ameeleza nia yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za kutoa misaada ya matibabu na kuahidi kurejea tena kwa ajili ya kuweka kambi ya matibabu ya macho.
Aidha Mganga mkuu wa wilaya ya Hai Dkt. Itikija Msuya ameeleza kuwa siku ya kwanza katika zoezi hilo walijitokeza zaidi ya watu 136 kupatiwa huduma ambapo wamegundua kuwa watu wengi wanasumbuliwa zaidi na magonjwa ya kisukari, presha, moyo na shinikizo la damu.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya hiyo Dkt Grace Ntogwisangu akitoa taarifa ya huduma za Afya kwenya hospitali hiyo ameishukuru taasisi ya misaada ya Al Ata'a kwa kuwezesha kutoa huduma za matibabu bila malipo kwa wananchi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai