Ukosefu wa heshima, mmomonyoko wa maadili, mila na desturi kandamizi na kukosa hofu ya Mungu vimetajwa kuchochea vitendo vya ukatili katika jamii nyingi.
Akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Hai kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili, mkuu wa divisheni ya Mipango wiaya hiyo Said Abdallah amesema kuwa ni jukumu la kila mmoja kuchukua hatua kwa kupaza sauti kupinga vitendo vya ukatili ili kupunguza na hatimaye kutokomeza vitendo hivyo.
"Ni jukumu la kila mmoja kupaza sauti kupinga vitendo vya ukatili viavyotokea kwenye jamii hasa majumbani, kwenye taasisi mbalimbali,shuleni, kwenye usaafiri wa umma na sehemu ambazo si salama kwa wananchi"
"Matukio ya ukatili wa kijinsia bado yapo na yanatokea kwenye maeneo mbalimbali katika wilaya yetu ya Hai licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kukomesha vitendo hivyo vinavyofanywa na watu wasiokuwa na mapenzi mema na wanawake na watoto"
"Natoa rai kwa kila mwananchi, sote tukatae ukatili wa aina yoyote pamoja kutoa ushirikiano pale uaktili unapotokea ili mhanga apate usaidizi mapema hususani matibabu na msaada wa kisheria lakini pia msababishaji achukuliwe hatua za kisheria, kwani kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza na kuondoa vitendo vya ukatili"
Kwa upande wake mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii wilaya ya Hai Robert Mwanga akisoma risala kwa mgeni rasmi ameeleza kuwa licha ya changamoto, halmashauri ya Hai kwa kushirikiana na wadau katika kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wamefanikiwa kuwajengea wananchi na jamii uelewa wa kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
"Elimu ya mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia katika ngazi ya vitongoji na kata imetolewa kwa njia ya mabango, vikao shuleni, na kwenye vyombo vya habari ikiwemo Redio Boma Hai fm"
Aidha ameeleza kuwa katika kutoa Elimu ya kupinga ukatili, jumla ya watu 17,461 wamefikiwa kwa njia mbalimbali ikiwemo shule za msingi, shule za Sekondari, mikutano ya vijiji na Redio Boma Hai fm.
Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Kila Uhai una thamani, tokomeza mauaji na ukatili kwa Wanawake na Watoto" yamehitimishwa Disemba 10 katika eneo la Kwasadala na kuhudhuriwa na wananchi, taasisi za kupinga ukatili na viongozi mbalimbali akiwemo diwani wa kata ya Masama kusini Cedrick Pangani.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai