Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Shabaha yenye urefu wa kilomita 0.59 na inayojengwa kwa kiwango cha lami katika Kata ya Muungano, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro mradi huu umegharimu zaidi ya shilingi milioni 300.
Barabara hiyo inatarajiwa kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wakazi wa kata ya Muungano na maeneo jirani, huku ikichochea shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa eneo hilo.
Aidha, ujenzi huo ni sehemu ya mikakati ya serikali ya kuimarisha miundombinu vijijini na mijini ili kuchochea maendeleo endelevu.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi huo kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 Ismail Ali Ussi amesema ujenzi wa barabara hiyo ni jitihada za serikali na kwamba ni mradi wa kimkakati inayoendelea kutekelezwa kote nchini.
"Mwenge wa Uhuru umefika hapa kujionea mradi huu wa kimkakati,na Leo hii wapo wengi ambao hawakutarajia barabara hii kujengwa Kwa kiwango cha lami lakini hayo yamewezekana kupitia serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan"Amesema Ismail Ussi.
Wananchi wa Hai wameonyesha furaha yao kwa ujio wa Mwenge wa Uhuru na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuendeleza na kulinda miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai