Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 umekimbizwa katika wilaya ya Hai tarehe 09 Juni 2021 ukiwa na kauli mbiu ya TEHAMA ni Msingi wa Taifa Endelevu; Itumie kwa Usahihi na Uwajibikaji.
Ukiwa katika Wilaya ya Hai; Mwenge wa Uhuru umepitia miradi 7 yenye thamani ya shilingi 2,801,039,118.50 ambapo mradi mmoja ukiwekewa mawe ya msingi, miradi 4 imetembelewa na kukaguliwa maendeleo yake na mmoja kuzinduliwa.
Utekelezaji wa miradi hii umachangiwa na Serikali kuu shilingi 2,268,294,853.50 huku wahisani wakichangia shilingi 440,018,765 huku halmashauri ya wilaya ya Hai ikiweka shilingi 34,000,000 na nguvu ya wananchi ikifikia shilingi 54,725,500.
Pamoja na miradi hiyo; Mwenge wa Uhuru umetembelea na kukagua mradi wa kuboresha shughuli za utangazaji katika kituo cha Redio Boma Hai inayomilikiwa na halmashauri hiyo.
Akizungumza na wananchi kupitia redio; kiongozi wa Mbio za Mwenge Luteni Josephine Mwambashi ameipongeza Wilaya ya Hai kwa kusimamia kwa vitendo kauli mbiu ya Mwenge kwa kutumia redio hiyo kama chombo cha kuboresha maisha ya wananchi.
Awali akisoma taarifa ya uboreshaji wa urushaji wa matangazo ya redi Boma Hai; Mratibu wa redio hiyo Riziki Lesuya amesema uboreshaji huo ni matokea ya ushirikiano wa karibu kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Amesema UNESCO imeipatia redio hiyo vifaa vya Studio ya Matangazo (Broadcasting Studio), Studio ya Kuandalia Vipindi (Production Studio) na vifaa vya kurushia matangazo (Transmission Equipment) ambavyo vitaimarisha shughuli za utangazaji na kufanya redio isikike kwenye eneo kubwa na kuwafikia wasikilizaji wengi zaidi.
Mwenge wa Uhuru Maalumu walikimbizwa na kukesha katika Wilaya ya Hai na hatimaye kukabidhiwa katika Wilaya ya Siha kuendelea na safari ya kusambaza nuru kwenye wilaya zote za Tanzania kuimarisha umoja wa kitaifa, upendo na uwajibikaji lakini zaidi kuimarisha maendeleo ya wananchi kwa miradi mbalimbali.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai