Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Abdalla Shaib Kaim ameeleza kuridhishwa na ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya sekondari Hai (Hai day) ambayo imejengwa kwa gharama ya shilingi 64,285,000
“baada ya kupokea taarifa ya mwenge wa uhuru tumefanya ukaguzi wa kina kuhusiana na nyaraka mbalimbali zinazohusiana na mradi sambamba na kutembelea, kujionea na kukagua mradi wenyewe husika"
“kwa dhati kabisa niseme baada ya zoezi la ukaguzi ambalo tumelifanya hapa niwasifie sana kwa upande wa nyaraka zote ziko vizuri, pia kwa upande wa mradi wenyewe itoshe kusema Mhe. mkuu wa wilaya kwenye mradi huu umeupiga mwingi sana”
“mradi mzuri, majengo yanavutia, na kikubwa ambacho mmekifanya baada ya kukamilisha ujenzi wa madarasa matatu kuna kiasi cha fedha ambacho kimebakia mkajiongeza mkajenga na ofisi, hongereni sana nyinyi ni wazalendo na mmeendelea kutumia fedha vizuri hongereni sana”
Hata hivyo kiongozi huyo wa mbio za mwenge alipokuwa akizungumza kwenye mradi wa uoteshaji wa mbogambaga na matunda Youth Green Movement uliogharimu kiasi cha shilingi 31,000,000 ambapo kati fedha hizo 20,000,000 ni mkopo usiokuwa na riba kutoka halmashauri, ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Hai kwa kuendelea kutekeleza agizo la serikali ikiwa ni pamoja na kutumia 10% ya mapato yake ya ndani katika kuwezesha makundi maalum
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai