Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Diwani wa Kata ya Muungano Mhe. Edmund Rutaraka amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa madiwani wa halmashauri hiyo ili kwa pamoja washirikiane kuwahudumia wananchi wa wilaya hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano wa kujitambulisha kwa watumishi wa halmashauri hiyo, Rutaraka amesema madiwani waliochaguliwa siyo malaika na kwamba hawaji kuleta miujiza bali ni wanadamu ambao kwa kushirikiana na watendaji waliopo wanaweza kuiletea manufaa kwa hamashauri na wananchi wake.
Rutaraka amesema ameamua kukutana na watumishi ili kujitambulisha na kuwaeleza watumishi matarajio ya madiwani na kuweka mikakati ya namna bora ya kuwahudumia wananchi.
“uwepo wetu ni kuwahudumia wananchi. Tunataka wananchi waone tofauti ya miaka mitano ya 2020 hadi 2025”
“Wananchi watambue tofauti la baraza la madiwani linaloongozwa na Chama cha Mapinduzi na mabaraza mengine. Ni lazima tufanye kazi kwa bidii kutatua changamoto za wananchi kwenye halmashauri yetu” Amesisitiza Rutaraka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amemhakikishia Mwenyekiti huyo kuwa ofisi ya Mkurugenzi pamoja na watumishi wote wa halmashauri hiyo wapo tayari kushirikiana na madiwani katika kuwahudumia wananchi.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikuhakikishie kuwa ofisi yangu na watumishi wote walio chini yake wapo tayari kushirikiana nawe na baraza lako katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwahudumia wananchi wa Hai” Amesema Sintoo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai