Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka ambaye pia ni diwani wa kata ya Muungano amewashauri wataalamu wa halmashauri ya wilaya hiyo kuongeza nguvu zaidi pamoja na ushirikiano katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia malengo kusudiwa waliyojiwekea ikiwemo kutoa huduma mbalimbali kwa jamii.
Rutaraka ameyasema katika kikao cha robo ya nne ya mwaka cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo ambapo mbali na kupongeza jitihada za dhati katika zoezi la ukusanyajj wa mapato pia amesema ni vyema wataalamu wakazidi kushirikiana ili kutorudi nyuma katika ukusanyaji wa mapato na badala yake washirikiane na madiwani katika kuibua vyanzo vipya vya mapato.
Naye Afisa tawala wa wilaya Hai Bi. Marry Mnyawi akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa amesema kuwa ukusanyaji wa mapato uendana sambamba na usimamizi madhubuti ya miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa ili kuleta tija kwa wananchi.
Kwa upande wake Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Hai Ndg. Gunda amewataka madiwani kutambua kuwa wanao wajibu mkubwa wa kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zao kwani miradi hiyo lengo lake ni kuwanufaisha wananchi huku akitolea mfano ujenzi wa chuo cha VETA katika kata ya Bondeni ambapo tayari zimekwishaletwa fedha zaidi ya Mil. 200 na kuwaraka madiwani kushiriki katika kuzuia mianya ya rushwa na ubadhirifu.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myingaamesema kuwa kwa mwaka huu mpya wa fedha kipaumbele kikubwa ni kuhakikisha kuwa wanasimamia vyema suala la ukusanyaji wa mapato pamoja na usimamizi wa fedha za miradi inayotekelezwa katika wilaya ili miradi hiyo iweze kulera tija kwa wananchi kama ilivyo azma ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai