Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya hai ambaye pia ni diwani wa kata ya muungano mjini bomang'ombe mhe. Edmund rutaraka leo machi 4 2021 amekabidhi mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi shabaha iliyopo katika kata hiyo.
Akikabidhi mifuko hiyo ya saruji katika kikao kilichowakutanisha wananchi wa mtaa huo na viongozi wao, rutaraka amesema kuwa hiyo ni sehemu ya ahadi yake aliyoahidi kwa wananchi wakati wa kampeni.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mchango huo amewataka wananchi na viongozi wa mtaa huo kujitolea kwa hali na mali kufanikisha ujenzi huo na kuwa serikali inamchango wake ambao utasaidia kukamilisha kwa %100 ujenzi huo na kuondoa changamoto hiyo.
Ameongeza kuwa halmashauri ya wilaya ya hai inalengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanasoma katika mazingira mazuri kwa kuanza kukarabati pamoja kuongeza vyumba vya madarasa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ujenzi shuleni hapo bw.godson abraham amesema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa madarasa hali inayosababisha baadhi ya wanafunzi kusomea nje na msimu wa mvua wanafunzi kushindwa kusoma.
Nao wananchi wa mtaa huo wamempongeza diwani huyo kwa juhudi zake za kuisaidia jamii yake kwakutoa michango ya aina mbalimbali ikiwemo kwenye elimu.
Diwani huyo pia ametumia nafasi hiyo kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wake ambapo ameahidi kwenda kuzifanyia kazi
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai