Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania wilaya ya Hai ambaye pia ni Mkurugenzi washirika la Gaeso Bi Hapyness Eliufoo ametoa pongezi kwa watumishi wa divisheni ya Maendeleo ya Jamii na serikali kwa ujumla kwa kuleta mpango wa malezi ya watoto katika wilaya ya Hai.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa programu jumuishi ya taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Hai ambapo amesema wanawake sikuhizi wameacha utaratibu wa malezi ya mtoto suala ambalo limechangia kuporomoka kwa maadili.
Eliufoo amesema mpango huu umekuja wakati muafaka na ukitekelezwa vema utapunguza au kumaliza changamoto ya maadili katika jamii na kuwataka wadau wote wanaotakiwa kushiriki katika mpango huu kutekeleza wajibu wao kwa maslai ya taifa.
Pamoja na hayo ameshauri kiundwe kikundi kwenye kata, na vijiji kuhusu swala la malezi na vikundi hivyo vijengewe uwezo ili vitoe huduma katika jamii.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai