Naibu waziri wa Ardhi Angelina Mabula ameipongeza wilaya ya Hai kwa juhudi zinazofanyika za kutatua migogoro ya ardhi na kuagiza kuendelea kuweka tutaratibu maalumu wa kutatua migogoro ya ardhi kwa muda mfupi ili wananchi waendelee kunufaika na ardhi wanayomiliki.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Hai Mabula amesema pamoja na kusikiliza kero za ardhi na kuzitatua pia utoaji wa hati miliki kwa wananchi kwa wakati utasaidia kupunguza malalamiko ya ardhi .
Amewaagiza watumisi wa idara ya ardhi kuwapatia wananchi hati mmiliki za ardhi kila mwananchi aliyoomba ili kuweza kumiliki eneo lake na kuwa salama pamoja na kuweza kulitumia kma fursa ya kujipatia mikopo ya aina mbalimbali
Naye mkuu wa idara ya ardhi wilaya ya Hai, Jacob Mhumba amesema kuwa kutokana na umuhimu mkubwa uliopo katika ardhi wamekuwa wakipata changamoto ambazo zinatokana na kutokupata mafunzo kwa wataalamu wa ardhi hali ambayo inafanya kutokea kwa makosa mbalimbali pamoja na ufinyu wa bajeti uliopo ambao unaathiri utendaji wao wa kazi.
Pia amemshukuru Mkuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama wilaya kwa ushirikiano uliofanikisha kutatua migogoro ya ardhi kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza katika ziara hiyo mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole sabaya amesema kuwa amekuwa akilipa uzito suala la migogoro ya ardhi ambapo amefika mikutano ya kusikiliza na kutatua kero za ardhi pamoja na miradhi ambayo anayo kwa kiasi kikubwa ilitawaliwa na masuala ya ardhi.
Hata hivyo Naibu Waziri Mabula amefafanua kuwa malengo ya ziara yake mkoani Kilimanjaro ni kufuatilia upimaji wa taasisi za umma,kudhibiti ujenzi holela wa makazi ,migogoro ya ardhi pamoja na kuhakikisha watu kuwa na hati za umiliki wa ardhi zao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai