Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. David Silinde amefanya ziara ya kikazi ya siku moja wilayani Hai na kupongeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Silinde ametoa pongezi hizo akiwa katika kijiji cha Shirimatunda na kushiriki shughuli za ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Shirimatunda iliyopo kijijini hapo ambapo ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule hiyo.
Amesema kuwa kwa kasi ya ujenzi wa shule hiyo inaonesha kuwa hadi kufiki Mei 30 mwaka 2022 ujenzi wa shule hiyo utakamilika kama ilivyokusudiwa ili kusaidia wanafunzi wa eneo hilo kupata huduma ya elimu karibu na eneo hilo.
Awali akimshukuru naibu waziri kwa kushiriki katika ujenzi huo, diwani wa kata ya Mnadani Nasib Mndeme amemuomba naibu waziri kufikisha salamu zake za shukrani kwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa kupatikana kwa shule hiyo kunakwenda kutatua changamoto za umbali waliokuwa wakitembea wanafunzi wa eneo hilo ambapo wanafunzi wa eneo hilo wanalazimika kutembea umbali wa Zaidi ya km 12 kuifika shule ya sekondari Mailisita inayotumika kwa sasa.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga maesema kuwa kwa sasa serikali imeshatoa kiasi cha shilingi milioni 470 kati ya milioni 600 ambayo ilitengwa kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai