Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Kazi, Bunge, ajira na walemavu Jenista Mhagama ameziagiza halmashauri zote za wilaya nchini kuhakikisha wanatumia vyema teknolojia zinazopatikana kwenye maonesho ya nanenane katika kuwafaidisha wakulima kwenye maeneo yao.
Pia amewataka Maafisa Kilimo kuhakikisha kuwa wanaendelea kutoa utaalamu wa kilimo katika mabanda ya Nanenane hata baada ya maonesho hayo kukamilika ili wananchi waweze kufaidi utaalamu wao muda wowote wanapohitaji.
Akifunga maonesho ya nanenane kwa mikoa Kanda ya Kaskazini; Waziri Mhagama amesema kuwa ipo haja kwa kila kanda kunapofanyikia maonesho ya Nanenane kuandaa wataalamu wa kilimo ambao watakuwa wakiendelea kutoa huduma hizo hata baada ya maonesho hayo kumalizika
Mhagama amesema kuwa asilimia 65 ya malighafi za viwanda hutokana na mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi hivyo ni lazima kazi ya kutoa elimu ya maswala hayo kuwa endelevu na kupewa kipaumbele.
Maonesho ya Nane Nane ya 2018 kitaifa yamefanyika mkoani Simiyu na yanabebwa na kaulimbiu “Wekeza katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Maendeleo ya Viwanda.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai