Ummy Hamis Nderiananga. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderinanga, amefanya ziara yake katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambapo ametembelea miradi inayofanywa na Umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo.
Mh Nderinanga amefika katika kijiji cha kimashuku kata ya Mnadani ambapo ameshuhudia ujenzi wa jengo la UWT linalojengwa na umoja huo pamoja na ujenzi wa zahanati unaoendelea kijijini na kuchangia matofali 500 kwajili ya ujenzi wa jengo la UWT na mifuko 50 ya sementi kwa ajili ya zahanati hiyo.
Pamoja na hayo amewahimiza viongozi kuandaa warsha kwa ajili ya walemavu nakupata changamoto zao ili wilaya iweze kusimamia changamoto hizo na kuzitatua
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kijiji cha kimashuku kata ya Mnadani Selestine Mkude amemshukuru Naibu Waziri kwa kuunga mkono jitiada za ujenzi unaoendelea kijijini apo.
Hata hivyo Mh Mbunge wa wilaya ya Hai Mh sashisha Mafue amesema kazi yake kubwa aliyonayo katika kijiji hicho cha kimashuku nikuhakikisha maji na umeme vinafika na hilo atalitekeleza kwa uwadilifu.
Nae mkuu wa wilaya ya Hai Mh Amiri Mkalipa amezidi kusisitiza maendeleo kwa wakina mama na kuahidi kuwaunga mkono katika jitiada za maendeleo
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai