Jeshi la Polisi katika wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro limesema kuwa limejipanga imara kukabiliana na wale wote watakaokuwa na nia ovu ya kufanya vurugu na kuhatarisha amani katika kampeni za vyama mbalimbali za siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Inspekta Shabo Pamoja na Inspekta Malimba kutoka jeshi la polisi Hai wakati wakizungumza katika kipindi cha Siku Mpya kinachorushwa na Radio Boma Hai chenye lengo la kutoa elimu ya usalama wa raia na mali zao pamoja na amani .
Amebainisha kuwa makundi yote ya ovyo ambayo yamejiandaa kwa ajili ya kuleta vurugu yatashughulikiwa na kazi ya jeshi la polisi ni kulinda amani ya Tanzania na maliza za watanzania.
Katika hatua nyingine Inspekta Shabo amesema kuwa jeshi la Polisi litahakikisha linafuatilia kwa makini mwenendo wa kampeni.
Pia kwa pamoja wametoa wito kwa watanzania kuacha watu wa kulinda nyumba pindi wanapokwenda kwenye shughuli mbalimbali ili pasitokee uhalifu wowote na jeshi la polisi litahakikisha lina linda usalama wa mali na wananchi wake.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai