Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amepokea barua za wenyeviti 20 wa vijiji na vitongoji waliojiuzulu nafasi zao kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Akizungumza ofisini kwake mapema leo, Sintoo amesema amepokea barua hizo 20 zilizoandikwa na wenyeviti hao kila mmoja akimtaarifu uamuzi aliouchukua wa kuachia nafasi zao kwenye cha hicho.
“Asubuhi ya leo hii nimepokea barua 20 za waheshimiwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambao wameniandikia kuhusu kujiudhulu nafasi zao za uenyekiti huku wakihama kutoka chama cha CHADEMA na kwenda CCM. ” Amesema Sintoo.
Kwa upande wake Nasoro Mushi aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Wari Sinde ambaye pia alikuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Hai amebainisha kuwa amefanya uamuzi huo kwa ridhaa yake baada ya kuona kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya CCM.
“Mimi kuhama chama cha siasa ni swala la kawaida, halikuanzia kwangu wala halitaishia kwangu kwani ni haki ya kikatiba kwa mwananchi kuchagua chama anachokiunga mkono”. Amesisita Mushi.
Naye Menyekiti wa Kijiji cha Kyuu Moses Munuo amesema ameamua kuhamia CCM kwa sababu serikali iliyopo madarakani inafanya kazi yake vizuri kuwatumikia wananchi.
“Kazi kubwa ya upinzani ni kupinga mambo wanayofanyiwa wananchi bila wenyewe kufurahi; mimi binafsi nimeona juhudi za Rais John Magufuli za kunyoosha yale yote tuliyokuwa tunayasema majukwaani ambayo sasa hatuna haja tena kwani yanatekelezwa vizuri” Amesisitiza.
Akithibitisha azma yake Godfrey Kivuyo aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji cha Jiweni na Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Bomang’ombe amesema kuwa kazi ya uongozi ni kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo kitu anachoamini atakifanikisha vizuri akiwa ndani ya CCM.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai