Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amemtaka Mkuu mpya wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya kuwatumikia wananchi wa Wilaya ya hai na kutatua changamoto zilizopo nndani ya wilaya ili kuendana na kiapo alicho apa.
Ameyasema hayo leo wakatia wa Kumuapisha Mkuu huyo wa Wilaya ya Hai Mjini Moshi mara baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia John Pombe Magufuli wiki hii.
Mghwira amemtaka mkuu huyo wa wilaya kushughulikia migogoro ya wafugaji na wakulima inayo ibuka katika wilaya ya Hai, kushughulikia na kusimamaia ipasavyo vyanzo vya mapato vilivyopo ndani ya wilaya pamoja na kutatua changamoto zinazo jitokeza katika sekta ya elimu na afya.
Mara baada ya kuapishwa, Mkuu huyo wa Wilaya Lengai Ole Sabaya amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini kuwa anaweza kusimamaia na kuongoza wananchi wa Hai na kuahidi kutekeleza kazi zote na kuwa muaminifu kwa rais na wananchi wa Wilaya ya Hai.
Sabaya amesema kuwa kupitia ilani ya chama cha mapinduzi, ilani hiyo itaenda kutekelezwa kwa kushirikiana na kamatia ya ulinzi na usalama ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele ili kufikia lengo linalo hitajika.
Aidha amemshukuru Mkuu wa Mkoa Anna Mghwira kwa kumgusia changamoto zilizopo ndani ya wilaya ya Hai na kumpa nafasi ya kufahamu wapi pa kuanzia kuziondoa changamoto hizo.
Lengai Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai