MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira amesema kuwa serikali inaridhishwa na makusanyo na matumizi ya fedha za Bima ya afya ya hospitali ya wilaya ya Hai.
Akizungumza wafanyakazi katika sherehe za sikukuu wafanyakazi kimkoa iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika ,amesema anaridhishwa na matumizi ya fedha yanayofanywa na wataalamu wa wilaya hospitali hiyo.
Dkt Mghwira amesema ,hospitali hiyo imeweza kutumia fedha ya Bima ya afya kujenga vyumba nne ambazo vitatumika kwa matumizi mbalimbali pamoja na wodi ambazo zitasaidia kuboresha huduma ya afya pamoja na kuondoa msongamano wa wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
Katika hatua nyingie mkuu huyo wa mkoa amesikitishwa na utoaji wa huduma za afya usiodhirisha kwa hospitali za Rufaa ya Mawenzi na KCMC ambao umekuwa ukilalamikiwa na wananchi pamoja na wageni wanaotoka nje ya nchi.
Dkt Mghwira amesema hospitali hizo zimekuwa zikitoa huduma kibaguzi ,kizembe ,ubadhirifu na pia amesikitishwa na kiasi kikubwa kinachotozwa kwa wageni wanaofika kupata huduma za kiafya ambapo huchajiwa kiasi cha dola 250 wakati wa kufungua jadala la matibabu
Hata hivyo amezitaka halmashauri zote mkoani Kilimanjaro kuwa na tabia za kutumia fedha zinazopatikana kuboresha huduma za kijamii badala ya kuendelea kusubiri utekelezaji wa miradi kutoka serikalini.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai