Jamii ya wamasai wilayani Hai wamepongezwa kwa kuendelea kuwa na maadili sahihi katika jamii.
Pongezi hizo zimetolewa na mbunge wa Jimbo la Hai Mh,Saashisha Mafuwe katika sherehe za kusimika wateule wa mila(Maleguwanani) wa ukoo wa Laizer zilizofanyika katika Kijiji Cha Tindigani kata ya KIA.
Mh,Mafuwe amesema kuwa maaadili mema huleta sifa kwa mwenyezi Mungu.
"Kama Kuna jamii hapa duniani iloyobaki na maadili sahihi yanampa sifa mwenyezi Mungu Ni sisi wamasai" alisema Mafuwe.
Pia amewataka wanaume wa jamii ya kimasai kuwapeleka watoto wa shule kwani hafurahishwi kuwa kiongozi wa jamii ya watu wasio kwenda shule.
"Wakina mama watoe adhabu kwa kina baba,mkirudi nyumbani jioni wanawake ngumu,mimi sifurahishwi kuogaza jamii ndogo ya ambao hawajaenda shule".
Aidha amesema kuwa wilaya ya Hai imepata miradi mingiikiwwmo vituo vya afya,shule,barabara nk.
"Tangu tumepata Uhuru wilaya ya Hai hatujawahi kupata miradi mingi Kama tulivyopata" alisema Mafuwe.
Kwa upanda wake diwani wa kata ya KIA Mh,Tehera Kipara amesema pamoja na kuwepo kwa maendeo katika kata hiyo kwa miaka minne wanasubiri kuanza na kukamilika kwa miradi mingine ikiwemo ujenzi wa shule ya veta na kituo Cha afya Cha KIA
"Kwa muda wa miaka minne tumejenga josho jipya na la kisasa,madarasa kumi na Kuna taasisi mbili ambazo serikali imeanza kukaagua maeneo ya kufanyia kazi na kazi imeshaanza"alisema Kipara.
Naye Luta Petro Laizer mwenyekiti wa UVCCM kata ya KIA na msemaji wa ukoo wa Laizer amempongeza Mh mbunge wa Jimbo la Hai kwa kuweza kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ifumbuzi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Rais Samia Suluh Hassan
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai