Mashindano ya Saashisha Cup 2022/2023 yaliyoanza rasmi mwezi Septemba 2022 kwa kuzikutanisha timu 87 kutoka ndani ya wilaya ya Hai yanaendelea katika vi- wanja mbali mbali.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Hai yanalenga kuin- ua na kuendeleza vipaji ususani kwa vija- na ambao wengi wao hukosa fursa za kuo- nesha vipaji.
Mpaka sasa mashindano hayo yamefikia hatua ya 20 bora baada ya kukamilika hatua ya awali na mbuge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafue alivipatia vilabu vyote vilivyoingia hatua hiyo vifaa vya michezo kwa timu seti moja ya jezi pamoja na mipira kwa ajili ya hatua ya 20 bora.
Kwa mujibu wa msimamizi wa mashindano hayo Omari Mlekwa alisema michezo ili- yofanyika wiki ya tarehe 19-25 Machi, katika viwanja mbali mbali vilikutanisha timu ya Homeboys na Paris ambapo home boys iliibuka na ushindi wa 1-0, michezo mingine ilihusisha timu za Kia na Kware ambapo timu ya Kware ilifanikiwa kutinga kumi bora baada ya kuifunga Kia bao moja, huku timu ya Kwasadala ikishindwa kutinga kumi bora baada ya kukubali kichapo cha goli moja kutoka kwa Lambo FC.
“Mshindano hayo yanaendelea vizuri mpaka yapo hatua ya 20 bora vilabu vi- kiumana kuhakikisha vinapata nafasi ya kuingia hatua ya kumi bora ambayo ita- fanyika wiki ijayo, nimshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Hai Mafue kwa kud- hamini mashindano hayo “Mbunge wetu amejua hitaji la vijana katika michezo kwani tulikuwa tunakabiliwa na changa- moto ya vifaa vya michezo lakini kwa sasa asilimia kubwa vilabu vimepewa vifaa hivyo.”
Mashindano yanaendelea katika viwanja mbali mbali wilayani hai ikiwa ni pamoja na Nkwamasi, Nkwakinini, Mailisita, Half London na Lambo Estate.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai