Viongozi wa chama cha ushirika wa akiba na mikopo cha walimu wilaya ya Hai na Siha (H.T. SACCOS) wametakiwa kuwa wawazi na waadilifu katika uendeshaji wa chombo hicho kama katiba inavyoelekeza ili kuepuka migogoro baina yao na wanachama.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa mkutano wa ishirini na mbili (22) wa chama uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya chama hicho.
“migogoro mingi huanzia kwenye fedha kwa kutokuwa waadilifu na wawazi katika uendeshaji wa shughuli za chama,katiba iheshimiwe, kutokusoma taarifa za mara kwa mara na ninyi wanachama lazima muwe wawazi katika uendeshaji wa shughuli zote na muwe waadilifu”Alisema Myinga
Myinga amewataka wanachama wanaodaiwa wajitahidi kulipa madeni yao ili Saccos iweze kuendelea kujiendesha yenyewe na wanachama wanaodaiwa kujitahidi kulipa madeni hayo kwa wakati ili kuepuka kutetereka kwa chama hicho.
“wanachama mnaodaiwa mjitahidi kulipa madeni yenu ili saccos yetu iweze kusonga mbele , hapa mlipo mpo mbali nawapongezeni sana ila lazima tujitahidi kufanya vizuri zaidi tusibweteke tukarudi nyuma”Alisema Myinga
Kwa upande wake mwenyekiti wa Saccos Baraka Owenya amewataka wanachama kukuza tabia ya kujiwekea akiba mara kwa mara , kukopa kwa busara na kulipa kwa wakati , na kuwataka wanachama kuendelea kuhamasisha watu wengine kujiunga na chama hicho
“bodi inawashukuru kwa dhati wanacahama wote wanaoonesha uzalendo mkubwa kwa chama na kuhamasisha watu kujiunga na chama chetu , pili napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru watendaji wote wa chama kwa kujitahidi kusimamia chama chetu kwa uaminifu na kupelekea chama kuendelea kutengeneza faida”
“pia nawashukuru wadau mbalimbali, mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya hai, na mrajisi wa vyama vya ushirika nchini , mrajisi msaidizi wa mkoa wa Kilimanjaro, maafisa ushirika hai na siha , maafisa elimu msingi na sekondari , chama cha walimu, shirikisho la vyams vya akiba na mikopo, saccos rafiki kwa ushirikiano wenu mkubwa katika kufanikisha shughuli za chama chetu”alisema Owenya
Naye mwenyekiti mstaafu wa chama hicho John Lengai amewataka wanachama kushirikiana ,kushikamana na kuwaamini viongozi ili Saccos iweze kusonga mbele
Mkutano huo wa ishirini na mbili(22) wa chama cha ushirika wa akiba na mikopo (saccos ) cha walimu wilaya ya Hai na Siha umeambatana na ugawaji wa vyeti kwa wanachama pamoja na upitishaji wa ajenda zote zilizojadiliwa.
Chama cha ushirika wa akiba na mikopo cha waalimu wa wilaya ya Hai na Siha kilisajiliwa mwaka 1993 na kuanza kufanya kazi mwaka 2001 kikiwa na wanachama 20 na mpaka kufikia mwaka huu wa 2022 kina wanachama 1407.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai