Serikali wilayani Hai mkoani Kilimanjaro imepiga marufuku shughuli zote za kilimo pembezoni mwa ziwa Boloti lililopo kitongoji cha Maiputa kijiji cha Kyuu eneo la kwa mma Sawa wilayani humo kufuatia moto mkubwa uliozuka na kuchoma sehemu kubwa ya nyasi kwenye ziwa hilo.
Akizungumza katika eneo la tukio Katibu tawala wilaya ya Hai Upendo Wella amewataka viongozi wa kijiji cha Kyuu kuweka utaratibu madhubuti wa kusimamia zoezi hilo ili kuhakikisha shughuli hizo zinasitishwa maramoja.
“Sheria ni msumeno mwenyekiti wa kijiji tuweke makubaliano ya pamoja tuzuie wasilime tena humu, kwa sababu wenzetu wa zimamoto pia wamefika ili kuhakikisha huo moto usiende kwenye mazingira ya watu na kuleta madhara makubwa”
Mashuhuda wa tukio la moto huo uliozuka majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo Novemba 9, 2021 wameeleza kuwa wafugaji waliokuwa wakichunga mifugo yao pembezoni mwa ziwa hilo ndiyo wanaosadikiwa kuwasha moto huo katika eneo hilo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kitongoji cha Maiputa katika kijiji cha Kyuu kata ya Masama Magharibi Benson Ndossy ameeleza kuwa alipokea taarifa kwa wakazi wa eneo hilo kuwa wamasai wamevamia na kuwasha moto kwenye ziwa hilo.
“Nilipata taarifa kwa raia walioko ukanda wa juu wakaniambia, mwenyekiti wamasai wameshawasha moto kule katikati waliokuwa wanachunga ng’ombe kule, tukawacheki wamasai wakatoa ng’ombe wakakimbia na zilikuwa ng’ombe nyingi sana”
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Kyuu Gerson Munuo ameeleza kuwa wameendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuzuia uharibifu wa mazingira lakini bado majanga ya moto na shughuli za kilimo ambazo zimekatazwa katika ziwa hilo bado ni changamoto.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai