Serikali imesema inatambua jitihada zinazofanywa na taasisi za dini pamoja na mashirika binafsi katika kuchangia suala la elimu hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari Jumuishi ya Mtakatifu Pamachius iliyojengwa na kanisa Katholiki; Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa jitihada za kuwekeza katika elimu zinazofanywa na mashirika ya dini na binafsi ni mchango tosha wa kusaidia elimu hasa katika kuyapa kipaumbele makundi maalumu.
Wakati wa uzinduzi huo Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali itatoa kiasi cha shilingi million kumi kusaidia kuendeleza miundombinu ya shule hiyo.
Amesema serikali imeboresha sekta ya elimu na tayari kwa sasa mazingira ya elimu yamezidi kuboreshwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za msingi elfu kumi na saba kwa shule za secondary pamoja na ujenzi unaoendelea katika chuo cha ualimu patandi cha jijini Arusha.
Waziri Mkuu amemwagiza Mkurugenzi wa halmashauri kutembelea shule binafsi zinazomilikiwa na taasisi za dini ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo na kushauri namna bora ya kuzitatua.
Aidha ameiagiza idara ya ukaguzi wa elimu kupitia na kukagua shule zote ili kuona kama zinakidhi vigenzo ikiwa ni pamoja na kuwa na mitaala sahihi inayotakiwa kutumika.
Naye Askofu wa Jimbo Kuu Katholiki Arusha muhashamu baba Askofu Isack Aman amesema kuwa kanisa liliona kuna hitaji la msingi la kujenga shule zenye kupokea wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuhakikisha kunakuwepo na fursa sawa kwa wote.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai