Baada ya kuwepo kwa kero ya muda mrefu oya kutokuunganishwa kwa umeme katika zahanati ya kijiji cha Ntakuja kata ya Kia wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro mkuu wa wilaya hiyo Lengai Ole sabaya amemuagiza meneja wa Tanesco wilayani hapo kuhakikisha zahanati hiyo inapata umeme mpaka ifikapo tarehe 11 septemba mwaka huu.
Sabaya ametoa agizo hilo leo Ijumaa 6.9.2019 wakati alipofanya ziara ya kikazi kijijini hapo ambapo walijitokeza wananchi waliotoa kero zao mbalimbali na kudai kuwa kukosekana kwa umeme na maji katika zahanati hiyo kunawafanya kukosa huduma muhimu za kiafya kwa wakati hali inayosababisha kutembea umbali mrefu kufuata huduma sehemu nyingine.
Mmoja wawananchi hao Mariamu athuman amesema "Kilio changu kikubwa ni kwamba zahanati yetu hatuna maji karibu akina mama wanakuja kujifungua, maji ni yakuchota visima vya jirani kwa hiyo mama zetu wanapata shida sana, mh Dc kwa hilo naomba utusaidie" Amesema.
Kuhusu kukosekana kwa maji ndani ya zahanati hiyo, sabaya amemtaka mwenyekiti pamoja na afisa mtendaji wa kijiji hicho cha Ntakuja kuhakikisha inapata maji huku akitoa kibali cha kuchangisha fedha kutoka kwa wananchi kijijini hapo zitakazo saidia kukamilisha zoezi hilo endapo italazimu kufanya hivyo.
Amesema "Hili jambo la maji namuelekeza mwenyekiti wa kijiji na afisa mtendaji simamia hili,na kibali cha kupata hiyo paipu kama mnachangisha nimekitoa hapahapa,kwahyo atakama mtaanza kuchangisha leo kibali nimeshakitoa chini ya mwenyekiti nunueni paipu pelekeni maji kwenye zahanati"amesema Sabaya.
Aidha amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya kuandika barua kwenda kwa uongozi wa Uwanja wa ndege wa KIA kwa niaba ya wananchi kuwaomba kwenda kufanya ukarabati katika zahanati hiyo kutokana na miundombinu yake kuwa chakavu.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho Bw. Daudi Moleli na Tauba Shabani wakizungumza baada ya Mkutano huo wameeleza kufurahishwa na ziara ya mkuu huyo wa wilaya kijijini hapo na kwamba imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wote wanaoishi kijijini hapo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai