MKUU wa wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameiomba wizara ya viwanda na biashara kukipatia kiwanda cha Kilimanjaro machine tools Manufacturs Company Limited kiasi cha shilingi bilioni 11 kwa ajili ya kukifufua kiwanda hicho kilichokuwa kikitengeneza mashine za aina mbalimbali hapa nchini
Ole Sabaya ametoa ombi hilo kwa wa Waziri wa Wizara hiyo Joseph Kakunda alipotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa na kiwanda hicho kilichopo kata ya Mnadani wilayani Hai
Alisema endapo wizara hiyo itakipatia kiasi cha fedha zilizotajwa zitasadia kuboresha miundombinu yake na kuweza kuzalisha mashine za aina mbalimbali ambazo zitasaidia kuongeza idadi ya viwanda vidogo na vikubwa pamoja na kuongeza ajira hapa nchini
“Mheshimiwa waziri kiwanda hiki kilikuwa tegemeo kwa uzalishaji wa mashine za aina mbalimbali lakini kutokana na uchakavu wa miundombinu wa umechangia kushindwa kufikia malengo yake ya kuzalisha mashine za kutosha kuhudumia jamii na kuinua uchumi wa nchini”
“Tena mheshimiwa waziri endapo kiwanda hiki kitaboreshwa katika miundombinu yake itaweza pia kutengeneza vipuri vya mashine za useremala, kusaga na kukoboa nafaka pamoja vifaa zitakavyotumika katika mashine za aina mbalimbalia ”alisema Ole Sabaya
Kwa upande wake, Maneja wa kiwanda hicho, Mhandisi Adriano Nyaluke alisema kuwa endapo miundombinu ya kiwanda hicho itaboreshwa itawezesha kuwapatia ajira zaidi ya elfu kumi kote nchini kutokana na kuzalisha na kutengeneza mashine zitakazoanzisha viwanda vidogo vidogo hapa nchini.
Mhandisi Nyaluke amesema wanalenga kupanua wingo wa bidhaa zitakazozalishwa na KMTC zitakazotumika katika sekta ya kilimo, usindikaji wa mazao na kuyaongeza thamani , mashine za kuwasaidia wachimbaji wadogo wadogo wa madini pamoja na mitambo ya kupasulia mbao
“Mheshimiwa waziri ili kuweza kukamilisha uzalishaji wa mashine mbalimbali kiwandani hapa kuna umuhimu wa ziada wa uzalishaji unaohitajika ikiwemo kuongeza mashine za kukunja na kupinda mabati yenye unene wa mm 6 pamoja na mtambo wa gesi wa kukatia vyuma vinene ”
“Pia mheshimiwa waziri ukarabati mkubwa unahitajika kwenye mfumo wa umeme wa kiwanda kwa kubadilisha nyaya zilizochakaa , vifaa vya uthibiti wa umeme na mafuta ya transformer na kubadili vifaa vya uthibiti wa umeme sehemu inayopokea umeme wa TANESCO”amesisitiza maneja huyo.
Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho Waziri Kakunda amesema serikali itakipatia kiwanda hicho kiasi cha fedha walichohitaji ili kuboresha miundombinu ya kiwanda hicho ambayo itasaidia kuongeza kuzalisha na kusambaza mashine ambazo zitasaidia kuongeza ajira kwa watanzania
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai